Muziki

Jay-Z aibuka na mabadiliko ya jina lake la muziki

NEWYORK : RAPAnguli wa Marekani Shawn Corey Carter maarufu Jay-Z ameibua gumzo kubwa baada ya kufanya mabadiliko madogo lakini yenye maana katika jina lake la kisanii, hatua inayotafsiriwa na wengi kama kurejea kwenye mizizi ya mwanzo wa safari yake ya muziki.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Jay-Z ameongeza tena alama ya umlaut (¨) katika jina lake, jambo ambalo limeanza kuonekana kwenye majukwaa ya kusikiliza muziki kama Spotify, Apple Music na YouTube, pamoja na mabango ya matamasha yake yajayo.

Mabadiliko hayo yanaripotiwa kuendana na kumbukumbu ya miaka ya awali ya kazi yake ya muziki, hasa albamu yake ya kwanza ‘Reasonable Doubt’ iliyotoka mwaka 1996, ambapo jina lake lilionekana likiwa na mtindo huo wa kipekee.

Jay-Z anatarajiwa kufanya maonesho makubwa katika Yankee Stadium mwezi Julai, pamoja na kushiriki katika tamasha la Roots Picnic mwezi Mei, ambapo jina lake jipya litakuwa sehemu ya utambulisho wa matukio hayo.

Aidha, hatua hii inaonekana kama sehemu ya historia yake ndefu ya kubadilisha mtindo wa jina lake mara kadhaa katika maisha yake ya muziki, ikiwemo kuondoa hyphen na kutumia mitindo tofauti ya uandishi katika vipindi tofauti vya kazi yake.

Mabadiliko haya madogo ya jina yanaendelea kuonyesha jinsi Jay-Z anavyochanganya ubunifu na historia yake ya muziki, huku akiendelea kubaki mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa duniani katika tasnia ya burudani.

Related Articles

Back to top button