Japan njia nyeupe Kombe la dunia 2026

SAITAMA, Timu ya taifa ya Japan huenda ikawa timu ya kwanza kufuzu kwa michuano ya fainali za kombe la Dunia la FIFA mwaka 2026 wakiungana na wenyeji Marekani, Canada na Mexico ikiwa wataifumua bahrain katika Uwanja wa Saitama uliopo jijini Saitama nchini Japan.
Wajapani hao watafuzu ikiwa watapata pointi 3 kwenye mchezo huo baada ya kuwa kwenye kiwango nzuri katika michezo ya kufuzu kwa fainali hizo kwa bara la Asia wakiwa vinara wa kundi C kwa pointi 16 walizopata kwenye michezo 6.
Timu hiyo imedondosha pointi 2 pekee katika kampeni hiyo ya kufuzu kwa kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Australia mwezi Oktoba mwaka jana huku wakiwa mbele ya Bahrain watakaocheza nao kesho kwa points 10.
Mchezo huo unatarajia kuvuta hisia za watu wengi ambao hufurahishwa na tabia njema na ustaarabu unayooneshwa na mashabiki wa timu hiyo inapokuwa inacheza.