Filamu

James Cameron: Sitoendelea na Avatar

NEW YORK: MUONGOZAJI na muandaaji maarufu wa filamu za kisayansi, James Cameron, amedokeza kuwa ana nia ya kumaliza mfululizo wa Avatar ikiwa sinema yake ijayo, ‘Fire and Ash’, haitafikia matokeo mazuri kimataifa.
Filamu hiyo inayofuata itakuwa sehemu nyingine ya mfululizo wa mafanikio kwa Cameron, mwenye miaka 71.

Akizungumza kwenye kipindi cha The Town na Matt Belloni, Cameron alisema: “Watu wanapendelea kuachana na mfululizo wa filamu zinazofuata. Isipokuwa ni ile filamu ya tatu ya Lord of the Rings. “Hii ni kilele cha hadithi, lakini huenda si jinsi umma unavyoiona.”

Filmmaker wa Titanic aliongeza kuwa Avatar: Fire and Ash itakuwa mwisho unaofaa wa mfululizo huo endapo itashindwa kufikia matarajio.

Alisema: “Nimekuwa katika dunia ya Avatar kwa miaka 20, actually 30, kwa sababu niliiandika mwaka wa 1995, lakini sikuwa nikifanya kazi nayo kwa kuendelea kwa miaka ile 10 za mwanzo.”

Ingawa Cameron yuko wazi kwa kuachia wengine kuiongoza filamu za nne na tano za Avatar, mwandishi huyo pia wa filamu ya Terminator alisisitiza kuwa atahusika kwa karibu sana ikiwa filamu hizo zitatengenezwa na mtu mwingine.

Alieleza: “Angalia, nina chaguo hapo. Kuna viwango ambavyo najiingiza. Naweza kuwa mzalishaji.

Filamu ya Avatar: Fire and Ash itakayoachiwa rasmi tarehe 19 Desemba 2025 – itachukua nafasi baada ya matukio ya filamu ya 2022, The Way of Water.

Filamu hiyo itafuata safari ya Na’vi Jake Sully (Sam Worthington), Neytiri (Zoe Saldana) na familia yao, huku wakikumbwa na tishio kubwa kutoka kwa kabila la ‘Ash People’ linaloongozwa na Varang (Oona Chaplin) na kuibua tena mapigano makali ya Pandora.

Wakati mshtuko wa hisia na wanajeshi wa zamani wanarudi, ushirikiano na kabila la Metkayina utajaribu kuonesha nguvu yao, imani, na ustawi wa maisha yao.

Cameron awali alionesha shaka kuhusu filamu ya nne ya Avatar baada ya kusema kuwa gharama za uzalishaji wa Fire and Ash zilikuwa zimepanda mno.

Amesema kwenye Variety: “Jambo kuu ni, je, tutaweza kupata faida na Avatar 3? Faida hiyo itakuwa kiasi gani?

“Labda tusubiri kidogo hadi tuweze kupunguza gharama. Gharama za uzalishaji zimepanda sana kwa miaka hii, hasa katika masuala ya VFX.

“Kila kitu kimepanda kwa kiwango kikubwa, na kunaanza kufunga filamu ambazo ningependa kuzitengeneza.”

Related Articles

Back to top button