Kwingineko

Inter Miami yatinga tena fainali

 

LIONEL Messi amechochea kurejesha mchezoni klabu yake ya Inter Miami kutoka kufungwa mabao 2-0 na kuishinda Cincinnati kwa mikwaju ya penalti 5-4 na kutinga fainali ya Kombe la Wazi la Marekani katika mechi ngumu jijini Ohio.

Messi alipiga krosi mbili maridadi zilizofika kwenye kichwa cha mshambuliaji Leonardo Campana zilizozaa mabao yaliyoikoa Miami katika dakika za mwisho hivyo kulazimu mchezo kwenda muda wa ziada timu hizo zikitoka sare ya 3-3.

Hiyo ni mara ya pili kwa Miami kufika hatua ya matuta katika kipindi cha siku nne baada ya kuifunga Nashville katika fainali ya Kombe la Ligi Agosti 19 na kunyakua taji hilo la kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Inter Miami itakipiga katika fainali ya Kombe la Wazi la Marekani Septemba 27 dhidi ya Houston Dynamo iliyoitoa Real Salt Lake kwa mabao 3-1.

Related Articles

Back to top button