Mastaa

Hidaya Njaidi: Patrick na Jenipher Kanumba sio wapenzi

DAR ES SALAAM: MAMA mzazi wa Othuman Mkaidi ‘Patrick Kanumba’, Hidaya Njaidi, amefafanua kuhusu uhusiano uliopo kati ya Patrick Kanumba na Jenipher Kanumba, akisema wawili hao sio wapenzi kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Hidaya amesema amewahi kuwauliza Patrick na Jenipher kama wana uhusiano wa kimapenzi au kama wana mpango wa kuwa wapenzi, lakini walimjibu kuwa wameamua kubaki kama kaka na dada ili kulinda ukaribu wao.

“Nimewahi kuwauliza Jenipher na Patrick, mna mahusiano au mnatamani kuwa kwenye mahusiano? Wakasema tunataka kubaki kaka na dada ili tuendelee kubaki milele,” amesema Hidaya.

Amesema uamuzi huo unatokana na kutaka kulinda uhusiano wao wa karibu, kwani wanaamini kuingia katika mahusiano ya kimapenzi kunaweza kuleta changamoto endapo watatofautiana au kuachana.

Kwa mujibu wa Hidaya, Patrick na Jenipher wanaona ni bora waendelee kuwa kaka na dada ili waweze kudumisha ukaribu wao kwa muda mrefu bila kuathiriwa na changamoto zinazoweza kujitokeza katika mahusiano ya kimapenzi.

Hidaya amesisitiza kuwa licha ya ukaribu wao, wawili hao hawajawahi kuthibitisha kuwa wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, bali wamechagua kuendelea na uhusiano wao kama kaka na dada.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo ukaribu wa Patrick na Jenipher umekuwa ukizua sintofahamu miongoni mwa mashabiki kwenye mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button