Hersi: Bado hajamsema,na Mtasema

DAR ES SALAAM: RAIS wa Yanga, Hersi Said amesema kikosi chao hakijakamilika kuwa tishio Afrika, wanafikiria kuongeza nyota wawili ambao walikuwa kwenye mipango yao.
Kwa mujibu wa Hersi amesema kuwa wachezaji hao walikuwa katika mipango yao kwenye dirisha kubwa lakini biashara hiyo haikukamilika wana imani dirisha dogo wataongeza kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi.
“Dirisha dogo tutarudi kuangalia kama tutaweza kukamilisha sajili zao, wakishafika ndio mtapata majibu maana ya timu kukamilika, kwa kuifanya Yanga kuwa tishio kwa Afrika,” amesema Hersi.
Kuhusu mchezo wa marudiano, amesema kutokana na marekebisho yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mkapa, mechi yetu ya marudiano dhidi ya Vital’O, haitachezwa uwanja wa Mkapa na sasa kucheza katika uwanja wa Azam Complex, Jumamosi,Agosti 24, majira ya saa 1:00 jioni.
“Mechi iliyopita wenzetu Vital O walisema watatunywa kama supu lakini tulifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4 -0, Lakini kwenye mchezo huu wa marudiano ni zamu yetu sasa kuwanywa wao kama supu,” amesema Rais huyo wa Yanga.
Akazidi kufafanua kuwa kila mchezaji anayecheza Yanga anatakiwa na timu nyingine Afrika, kwa sababu wana wachezaji bora sana katika kikosi chao na Clemet Mzize ni tegemeo la Taifa, makocha wawili waliopita Yanga (Nabi na Gamondi) wamempa nafasi.
“Mzize yupo kwenye mikono salama zaidi akiwa na jezi ya Yanga ana mengi ya kujifunza na alipo ni mahala sahihi kwake kwa maslahi ya timu ya Taifa. Malengo yetu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu ni tufike tena hatua ya Robo Fainali. Lakini kwenye maisha Mwenyezi Mungu hutoa zawadi, tukipata zawadi ya kufika Fainali na kuchukua Ubingwa basi tutashukuru, sasa tunahitaji Robo Fainali na tutapambana kufanikisha hilo,” ameeleza Hersi.