Africa

Hatuongei sana tunakwenda kufanya kazi-Nabi

KUELEKEA mchezo wa kufuzu Ligi ya mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Hilal ya Sudan Oktoba 8, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema klabu yake imejiandaa vyema kuhakikisha inapata ushindi kwenye mechi hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam leo kocha huyo amesema kwa sasa hakuna cha kuongea zaidi ya kwenda kufanya kazi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Suala la kuongea tumewaachia mashabiki kwa sababu tunajua wanachokitaka siyo maneno ni matokeo mazuri na tumejiandaa kufanya vizuri kuhakikisha furaha yao inakuwa ya kudumu kwenye mchezo huu” amesema Nabi.

Amesema wachezaji wake wote wapo tayari kupambana kwenye mchezo huo wakijiamini na kumheshimu mpinzani wao,

Nabi alikuwa kocha wa Al Hilal miaka saba iliyopita akiifikisha klabu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Winga wa Yanga, Tuisila Kisinda.

Wakati huo huo Nabi amesema anaweza kumtumia winga Tuisila Kisinda Oktoba 8 kutokana na sheria na kanuni za Shirikisho la Mpira Afrika(CAF) kumruhusu baada ya kupata leseni.

Akizungumza na Spotileo amesema anataka kumtumia winga huyo kutokana na uzoefu wake kwenye michuano hiyo.

“Nina machaguo mengi kwenye nafasi ya wachezaji wa pembeni kulingana na uzito wa mchezo nafikiria kuwaanzisha Kisinda na Morrison hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kutosha,” amesema Nabi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button