Kwingineko

Haaland asaka rekodi za Messi

MONACO: AKIWA na rekodi mpya ya Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyoiweka hivi karibuni, mshambuliaji hatari wa Manchester city Erling Haaland anaikaribia rekodi nyingine nyingine kwa kasi kubwa.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City mwezi uliyopita ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyetumia michezo michache zaidi kufunga mabao 50 kwenye michuano hiyo kwa bao lake moja dhidi ya Napoli. Alifikisha idadi hiyo katika mechi yake ya 49 na kuvunja rekodi ya Ruud van Nistelrooy ya mabao 50 katika michezo 62. Na sasa rekodi ya Lionel Messi iko mashakani.

Messi ndiye mchezaji aliyetumia michezo michache zaidi kufikisha mabao 60 katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya. Akifanya hivyo katika mechi 80. Mabao mawili ya Haaland dhidi ya Monaco usiku wa Jumatano yanamaanisha kuwa ana mabao 52 baada ya mechi 50 pekee akibakisha nane tu kufikia rekodi ya Messi.

Mabao ya Haaland yaliipa Man City uongozi wa mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Stade Louis II. Akiwafunga bao la kuongoza dakika ya 15 kabla ya Jordan Teze kusawazisha dakika tatu tu baadaye.

Haaland alifunga tena dakika ya 44, lakini Nico Gonzalez alikiponza kikosi hicho alipoadhibiwa kwa kumchezea vibaya Eric Dier eneo la hatari na mapitio ya VAR kuamua kuwa mkwaju wa penalti ambayo Eric Dier alifunga.

Sasa ana mabao 17 katika mechi 10 za klabu na kimataifa. Manchester City ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham mwezi Agosti katika mchezo pekee ambao Haaland hakuweza kufunga katika msimu huu.

Related Articles

Back to top button