Wasifu
Golikipa wa zamani Madrid afariki dunia
TIMU ya Real Madrid imetangaza kuwa golikipa wake wa zamani Miguel Angel Gonzalez amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.
Gonzalez alicheza Madrid kati ya mwaka 1968 na 1986 akishinda makombe nane ya ligi na mawili ya Uefa miongoni mwa mataji 16 akicheza michezo 346.
“Real Madrid, Rais wake na bodi ya wakurugenzi imehunishwa na kifo cha Miguel Angel Gonzalez, mmoja wa magolikipa hodari katika historia yetu, mkongwe wa Real Madrid na soka la Hispania,” imesema taarifa ya klabu hiyo.
Vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa Gonzalez alikuwa akiugua ugonjwa unaosababishwa na seli katika ubongo au mfumo wa neva kushindwa kufanya kazi kwa muda mrefu na hatimaye kufa.




