Wasifu

Walcott astaafu soka

THEO Walcott ametangaza kustaafu soka ya ushindani akiwa na umri wa miaka 34.

Winga huyo wa zamani wa Arsenal, Everton na Southampton amesema uamuzi “unatisha” lakini “anataka kujaribu mambo mengine mapya.”

Walcott anastaafu kufuatia miaka 23 ya michezo 397 Ligi Kuu England.

“Nastaafu rasmi kucheza soka. Inatisha sana, siwezi kusema uongo,” amesema Walcott.

Katika kipindi cha miaka 13 akikipiga The Gunners Walcott alishinda kombe la FA mara tatu pamoja na Ngao ya Jamii mara mbili.

Amecheza mechi 47 timu ya taifa ya England katika kipindi cha miaka kumi akifunga mabao nane.

Walcott alianza kucheza klabu ya Southampton akiwa na umri wa miaka 16 mwaka 2005 na kuwa mfungaji bao mwenye umri mdogo zaidi kwenye klabu hiyo katika mchezo dhidi ya Leeds United.

Alicheza mechi 21 Southampton akifunga mabao manne kabla ya kujiunga na kikosi cha kocha Arsene Wenger, Arsenal mwaka 2006.

Alicheza mechi 397 The Gunners akifunga mabao 108 kabla ya kutimkia Everton mwaka 2029 kwa dili la pauni milioni 20.

Walcott alicheza michezo 85 The Toffees akifunga mabao 11 kabla ya kurejea Southampton miaka miwili baadaye.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button