Kwingineko

“Goli 10 hazitupumbazi” – Kompany

MIAMI: Kocha wa ‘The Bavarians’ Bayern Munich Vincent Kompany amesema ushindi wa mabao 10-0 walioupata dhidi ya Auckland City ya New Zealand katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia la Klabu, hautawapumbaza watakapokabiliana na Boca Juniors ya Argentina katika mechi yao ya pili ya Kundi C alfajiri ya Jumamosi.

Kompany anasema Boca walionesha ni namna gani wanaweza kuwa tishio kubwa kwenye ‘transition’ walipokaribia kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Benfica kabla ya kuruhusu uongozi wa mabao mawili kwa moja kupotea katika sare ya 2-2 dhidi ya Wareno hao na

“Tunajua ubora wa mashindano. kila timu inayoshiriki hapa ni timu inayoshinda. Boca ni timu hatari sana kwenye ‘transition’. Wanaamini kwenye ‘moments’ zao. ‘spirit’ ya timu ni nzuri. Tunawaheshimu Boca. Lakini tunajitazama na tunataka kuleta ubora wetu kwenye mchezo huu.” – Kompany aliwaambia waandishi wa habari kuelekea mchezo huo.

Kompany aliendelea kusema kuwa yeye na timu wanafahamu aina ya uchezaji wa klabu za Argentina huku akisema baadhi ya wachezaji wa taifa hilo waliopo barani Ulaya wanamsaidia kujua aina ya soka la Argentina lakini wao kama Bayern wanataka kuwa wao na waoneshe soka sahihi.

Kompany hakusita kuonesha furaha yake juu ya urejeo wa kiungo mkabaji Jamal Musiala na beki wa kati Dayot Upamecano baada ya kuwakosa kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na majeraha. Mjerumani Musiala ambaye alifunga mabao 12 Bayern ikitwaa taji lao la 34 la Bundesliga, aliingia akitokea benchi na kufunga hat-trick dhidi ya Auckland Jumapili.

“Jamal Musiala na Dayot Upamecano hawajacheza kwa muda mrefu. Tuna furaha sana kwamba wamerejea na wko timamu. Muunganiko ni suala muhimu, na tunapaswa kuliangalia. Vinginevyo, kila mtu yuko sawa kwa 100%,” Kompany alisema.

Bayern wanashikilia usukani wa kundi C wakiwa na pointi 10 wakifuatiwa na Boca Juniors na Benfica wenye point 1 huku Auckland City FC wakiwa mkiani bila pointi yeyote na mzigo wa mabao 10.

Related Articles

Back to top button