Africa
Fountain Gate yaagwa

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amekabidhi bendera ya Taifa kwa timu ya shule ya Fountain Gate inayokwenda Afrika Kusini kwenye mashindano ya Shule za Afrika.
Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Aprili 5 hadi 8 kwenye uwanja wa Mfalme Zwelithini uliopo jiji la Durban.
Michezo ya kufuzu mashindano hayo ukanda wa CECAFA ilifanyika Tanzania Februari, 2023.