Filamu ya Ramayana yaweka rekodi ya bilioni 160

INDIA: FILAMU kubwa ya Kihindi, Ramayana, inayowashirikisha Ranbir Kapoor, Yash na Sai Pallavi, inatarajiwa kuanza kwa mapato ya takribani rupia crore 1,600 (karibu shilingi bilioni 160 za Tanzania), kwa mujibu wa makadirio ya wadau wa biashara ya filamu.
Licha ya ukubwa wa bajeti na usambazaji wake, filamu hiyo huenda isivunje rekodi za ufunguzi zilizowekwa na filamu nyingine kubwa za India.
Mauzo ya tiketi za awali yameonesha kuongezeka kwa kasi kadiri siku ya uzinduzi inavyokaribia.
Kufikia Novemba 4, mauzo ya awali nchini India yalifikia rupia crore 77 kwa wikendi ya kwanza, huku crore 33 zikiwa za siku ya kwanza. Katika masoko ya nje, mauzo yalifikia dola milioni 5.6, yakichangiwa pia na Marekani na Canada.
Wadau wanakadiria kuwa Ramayana inaweza kuingiza zaidi ya crore 80 nchini India siku ya kwanza, huku soko la kimataifa likichangia mapato makubwa. Hata hivyo, matarajio ya kufikia crore 2,000 siku ya kwanza yanaonekana kuwa magumu.
Kwa upande wa rekodi, filamu hiyo inatarajiwa kushindwa kuvuka mafanikio ya Pushpa 2 (crore 274), RRR (crore 223), Baahubali 2 (crore 214) na Dhurandhar 2 (crore 205). Hata hivyo, inatarajiwa kuipita KGF Chapter 2 iliyofungua kwa crore 159.
Ramayana imetayarishwa na Namit Malhotra kupitia Prime Focus Studios kwa kushirikiana na DNEG na Monster Mind Creations. Ranbir Kapoor anaigiza Rama, Sai Pallavi ni Sita, huku Yash akiigiza Ravana. Sehemu ya kwanza inatarajiwa kuachiwa Novemba 5, 2026, na sehemu ya pili mwaka 2028.




