Burudani

Fahy Vanny afunguka kuhusu Paula Kajala

DAR ES SALAAM: VIDEO Queen, Fahy Vanny, ameweka wazi kuwa hana ugomvi wowote na Paula Kajala na hawezi kukumbuka kama walishawahi kugombana hapo awali.

Akizungumza baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha akipishana na Paula Kajala kwenye hafla ya msanii Nandy, Fahy Vanny amekanusha madai kwamba alikuwa akimkwepa Paula.

Amesema hajui maneno hayo yametoka wapi na amesisitiza kuwa hana tatizo naye.

Aidha, Fahy Vanny ameweka wazi kuwa bado hajafikiria kuingia rasmi katika tasnia ya uanamitindo, licha ya kupokea simu nyingi za ushawishi kujiunga na sekta hiyo.

“Kwa kuwa napenda kuvaa na watu wanapenda mtindo wangu, niliwahi kupokea ujumbe kutoka kwa mbunifu wa mavazi wa msanii maarufu kutoka Marekani, Beyoncé. Tumekuwa tukizungumza mara kwa mara, na siku za mbeleni huenda tukashirikiana katika kazi,” amesema Fahy Vanny.

Habari hii inazidi kuibua mijadala mitandaoni huku mashabiki wakisubiri kuona maendeleo ya safari yake ya uanamitindo na mahusiano yake na mastaa wengine.

Related Articles

Back to top button