World Cup

EPL, LaLiga zatishia kususia CWC

MICHUANO ya Kombe la Dunia la Klabu (CWC) ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) 2025 imeripotiwa kuwa hatarini kususiwa na timu kutoka England na Hispania.

FIFA inayoongozwa na Rais Gianni Infantino ilitangaza mipango ya kuandaa mashindano ya timu 32 huko Marekani majira yajayo ya kiangazi kuamua klabu bora zaidi duniani.

Klabu kama Manchester City, Real Madrid na Chelsea zote zinatarajiwa kushiriki.

Hata hivyo, Mtendaji wa Premier League Richard Masters, Rais wa LaLiga Javier Tebas na Bosi wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa(PFA) Maheta Molango wana wasiwasi mkubwa kuhusu idadi kubwa ya timu zitakayochukua wachezaji na wametishia kuondoa timu zao iwapo michuano hiyo iliyofanyiwa mabadiliko haitarekebishwa.

Viongozi wote hao wanaunga mkono tishio la kususia na wanafikiria hatua za kisheria.

Molango amesisitiza kuwa FIFA ipo hatarini kuua mpira wa miguu kwa kuandaa michuano mwisho wa msimu mgumu.

“Mpira wa miguu unaua zao lake lenyewe,”ameema Molango.

Awali timu zilizokuwa zikishiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu zilikuwa hazizidi 7.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button