Kwingineko

Enrique ajutia vurugu kwa Chelsea

EAST RUTHERFORD, Meneja wa mabingwa wa Ulaya Paris St Germain, Luis Enrique amesema anajutiia kitendo chake cha kumsukuma mshambuliaji wa Chelsea Joao Pedro katika mzozo ulioibuka kati ya wachezaji na wakufunzi wa timu zote mbili kufuatia ushindi wa Chelsea wa 3-0 katika fainali ya Kombe la Dunia la Klabu usiku wa Jumapili.

Tukio hilo lilitokea wakati mlinda mlango wa PSG, Gianluigi Donnarumma alipokuwa akizozana na Joao Pedro, kabla ya Luis Enrique kuonekana kuinua mikono yake usoni mwa Mbrazil huyo akamsukuma na Joao Pedro akaanguka.

Baada ya Joao Pedro kuanguka meneja huyo wa PSG aliondolewa uwanjani na ukawa mwisho wa tukio hilo la ajabu lililoshuhudia wachezaji wa pande zote mbili na wakufunzi wao wakigombana.

“Mwishoni mwa mechi, kulikuwa na hali ambayo ninaamini ingeweza kuepukwa na kila mtu. Lengo langu na nia yangu, kama kawaida ilikuwa kujaribu kuwadhibiti wachezaji ili kusiwe na matatizo zaidi. Uwanjani huwa presha na mvutano mkubwa kwakweli najutia hilo.” – Luis Enrique alisema katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi.

Kocha huyo wa Mhispania alikiri ubaya wa tukio hilo na kuongeza kuwa atajitahidi kuhakikisha kuwa matukio kama hayo hayatatokea tena chini ya uangalizi wake ndani ya PSG

Related Articles

Back to top button