Nyumbani
Doumbia afiwa na baba mzazi

MCHEZAJI wa Yanga Mamadou Doumbia amefiwa na baba yake mzazi nchini Mali.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Yanga kupitia mitandao yake ya kijamii.
“Kwa niaba ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga uongozi wa klabu ya Yanga unatoa pole kwa mchezaji wetu Mamadou Doumbia na familia yake yote kwa msiba huu na Mwenyezi Mungu awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu,”imesema Yanga.
Taarifa ya Yanga imesema Doumbia anatarajiwa kusafiri leo asubuhi kwenda Mali kwa ajili ya kushiriki taratibu za mazishi.
Yanga imesema Mamadou Doumbia anatarajiwa kusafiri leo asubuhi kwenda Mali kwa ajili ya kushiriki taratibu za mazishi.