Burudani

Donald Glover afunguka kuhusu afya yake

LOS ANGELES: MWANAMUZIKI Donald Glover amefunguka ugonjwa mzito kumpata katika maisha yake, na kukiri kuwa na kiharusi tangu mwaka 2024 uliomfanya kumfanya kuhairisha show zake kwa mwaka mzima.

Glover ambaye pia ni mwandishi wa filamu, na mchekeshaji kupitia tamasha la Tyler the Creater Camp Flog Gnaw Festival lililofanyika Jumamosi usiku huko Los Angeles alisema nilipitia wakati mgumu sana wa kiafya.

“Nilikuwa na maumivu makali sana kichwani huko Louisisana hata hivyo sikuweza kuona vizuri, tulivyokwenda Houston nikaenda hospitalini na daktari akasema nina kiharusi”.

Glover amezidi kuwashirikisha mashabiki zake katika hili na kufunguka zaidi akisema walinikuta na shimo kwenye moyo wangu hivyo ikanibidi kufanya upasuaji mara mbili.

‘Mko na nafasi moja tu katika haya maisha, nakuwa muwazi maisha niliyoishi na nyie yamekuwa na baraka sana kwangu’ Golver azungumza hayo mwishoni mwa tamasha

Related Articles

Back to top button