Mastaa

Diamond: Nimemruhusu Lavalava aondoke

DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa bongo fleva Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amemruhusu msanii wake Abdul Idd ‘Lavalava’ aondoke na kujisimamia kwasababu ameishi naye vizuri kwa muda mrefu.

Diamond ameyasema hayo Dar es Salaam leo katika hafla fupi kati yake na kampuni ya Pepsi iliyokuwa ikitangaza kuendeleza ushirikiano mwingine na nyota huyo kama balozi wao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Diamond amesema nyota huyo ameishi naye kwa miaka nane bila matatizo n ani miongoni mwa wasanii anaowapenda.

“Hakunifuata kuniambia anataka kuondoka. Anajua nampenda sana. Ni kijana mwenye kipaji, mbunifu, anajituma. Nilimwambia kama anataka kuondoka aje nitampa ruhusa aondoke huru, tumeishi naye vizuri hajawahi kunivunjia heshima, tumeishi kwa kupendana,”amesema.

Alisema kutokana na nidhamu ya msanii huyo alimwambia kama kaka yake atamwezesha kiasi cha fedha cha kuendesha miradi yake.

“Wasanii waangalie makubaliano ni nini ni namna ya kuishi na watu. Suala la mikataba sio jambo kubwa ila ukitaka kujifanya wewe una kiburi watu watakuletea jeuri,”amesema.

 

Related Articles

Back to top button