Muziki

Diamond na Bien watikisa na “Katam”

DAR ES SALAAM:MWANAMUZIKI nyota wa Tanzania, Nassibu Abdul ‘Diamond platnumz’, ameachia rasmi wimbo mpya uitwao “Katam” akimshirikisha mwanamuziki mahiri kutoka Kenya, Bien Aime ‘Bienimesol’

Wimbo huu mpya umewasha moto mitandaoni na kuzua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wao wa muziki wa Afrika Mashariki.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Diamond aliwatangazia mashabiki wake kuhusu ujio wa kazi hiyo mpya ya muziki huku akitoa ujumbe mzito kwa mashabiki wa Uingereza ambako anatarajia kufanya onesho Ijumaa ya wiki hii.

“London, siwezi kusubiri kukuona Ijumaa hii katika ukumbi wa Royal Albert Hall.”

Ujumbe huo umeongeza hamasa kwa mashabiki wake walioko Uingereza ambao wanajiandaa kumpokea kwa shangwe kubwa katika tamasha linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii kwenye ukumbi maarufu wa Royal Albert Hall, jijini London.

Wimbo wa “Katam” unakuja ukiwa na mchanganyiko wa ladha ya kisasa ya Bongo Flava na Afro Soul, ambapo Bien anatoa mchango mkubwa kwa sauti yake maridhawa na uandishi wa mashairi wa hali ya juu, huku Diamond akisindikiza kwa mtindo wake wa kipekee uliomtambulisha kimataifa.

Hii ni kolabo ya kwanza rasmi kati ya Diamond na Bien, na tayari imepokelewa kwa kishindo na mashabiki waliokuwa wakingoja kwa hamu kuona mastaa hawa wakifanya kazi pamoja.

 

Related Articles

Back to top button