Denver Nuggests wana jambo lao NBA msimu huu

FAINALI ya tatu ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani “NBA” imemalizika katika mji wa Miami na kuacha simanzi kwa wenyeji wa mji huo baada ya timu yao kukumbana na kichapo.
Miami Heat wakiwa uwanja wa nyumbani wa FTX jijini Miami wamepoteza fainali ya tatu kwa kunyukwa na Denver Nuggets alama 109 kwa 94 na hivyo kuanza kufifisha matumaini yao ya kuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa msimu huu.
Nyota wa Denver Nuggets Jamal Murray na Nikola Jokic walikuwa mwiba mkali kwa Heat, ambapo Murray amefunga jumla ya alama 34 huku Jokic akifunga alama 32.
Kwa Matokeo hayo sasa Nuggets wanaongoza 2-1 na fainali ya nne itapigwa alfajiri ya Juni 10 na kama Nuggets watashinda tena basi watakuwa wameusogelea kwa karibu zaidi ubingwa.
Imeandaliwa na Antipas Kavishe