Kikapu
Dar City yaanza vyema michuano ya Afrika

DAR ES SALAAM:TIMU ya mpira wa kikapu ya Dar City imeanza vizuri kampeni zake za kufuzu kwa Basketball Africa League (BAL) 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa pointi 102–50 dhidi ya Djabal kutoka Comoros.
Mchezo huo umechezwa Jana usiku katika viwanja vya shule ya IST, vilivyopo Masaki, Dar es Salaam, ambapo Dar City ilionesha ubabe na kuutawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Leo Dar City itashuka tena uwanjan kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya kufuzu dhidi ya Blazers kutoka Uganda