Kwingineko

Cubarsi ashonwa nyuzi kumi

Kwa sasa anaendelea vizuri

Taarifa kutoka FC Barcelona zinaeleza kuwa beki wa klabu hiyo bwana mdogo Pau Cubarsi anaendelea vizuri baada ya kupata jeraha usoni lililotokana na kugongwa na mguu wa beki wa kati Uros Spajic wa Red Star Belgrade ya Serbia wakati wakiwania mpira wa kona ulioelekezwa langoni kwao.

Cubarsi mwenye miaka 17 alionekana kuvuja damu baada ya tukio hilo kabla ya kutolewa mnamo dakika ya 67 ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya Jumatano usiku Barcelona ikishinda mabao 5-2, mabao ya Robert Lewandowski aliyetupia mawili, Inigo Martinez, Raphinha na Fermin Lopez.

Kocha wa kikosi hicho Hansi Flick alisema kinda huyo alihitaji kushonwa na anaendelea vizuri kabla ya ukurasa rasmi wa klabu hiyo kuposti picha yake akitabasamu na ‘caption’ yenye maneno ya Kiingereza ‘I’m OK’ yaani niko sawa.

Pau Cubarsi ambaye ni zao la academia ya FC Barcelona ya La masia alianza kukitumikia kikosi cha kwanza cha FC Barcelona akiwa na miaka 16 katika mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Unionistas de Salamanca January 18, 2024. Tangu kipindi hicho amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu hiyo akileta ujuzi wa kileo unaotokana na kujiamini katika eneo lake.

Related Articles

Back to top button