
Msanii wa filamu nchini, Coletha Raymond maarufu kama ‘Coletha,’ amesema kuwa anaishi maisha yake kwa namna anavyotaka na hataki kupangiwa na mtu yeyote jinsi ya kuishi.
Coletha ametoa kauli hiyo baada ya kushambuliwa mitandaoni kufuatia picha zake akiwa kanisani huku amevalia suruali.
“Kuvaa suruali kanisani si dhambi. Kitu muhimu ni matendo yako, si mavazi. Na hata hivyo, suruali niliyovaa haikuwa imenibana, ilikuwa ya heshima,” amesema Coletha.
Akiendelea kujibu wakosoaji wake, alisisitiza: “Nawaambia watu wanaonizungumzia mitandaoni kuwa sipangiwi maisha. Ninaishi ninavyotaka, si kama wanavyotaka wao. Najua kuwa sijafanya kosa lolote.”
Aidha, Coletha ameongeza kuwa ni kawaida kwa watu kuzungumza au hata kuzusha mambo kuhusu wengine, lakini hilo halitomwathiri katika maisha yake.