Masumbwi

Choki ajipanga kurudi na kasi

DAR ES SALAAM:BONDIA Juma Choki amesema anajipanga kurudi kwa kasi kwenye michuano ya dunia hatua ya 16 bora inayofanyika Saudi Arabia.

Baada ya kuvuka mzunguko wa 32 bora, mabondia wamepewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea kwa ajili ya hatua inayofuata. Choki amesema atautumia muda huo kujiimarisha zaidi katika mazoezi ili awe tayari kwa pambano lijalo.

Akizungumza na SpotiLeo Choki amesema anataka kutumia muda aliopewa kupumzika kuendelea kujiimarisha kimazoezi kujiweka imara kwa pambano lijalo.

“Nitakaa nyumbani kama wiki tatu kisha baadaye nitarudi tena Dubai kujiandaa vizuri na maandalizi mengine, lengo langu ni kuhakikisha napambana kila hatua kufika fainali,”amesema.

Katika pambano la kwanza alimpiga bondia kutoka Ufilipino Bryx Piala katika mashindano hayo yaliyoshirikisha mabondia kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Choki alishinda kwa pointi za majaji watatu yaani 58-56, 59-55 na 59-55 katika pambano la hatua ya 32 bora.

Atakutana na bondia wa Mexico Hector Munguia ambaye yeye ametinga hatua hiyo baada ya kumchapa Idris Gbadamosi kwa TKO raundi ya sita.

Related Articles

Back to top button