Habari Mpya

Chelsea yamfukuza kazi Tuchel

KLABU ya Chelsea “The Blues” imetangaza kumfukuza kazi Kocha Thomas Tuchel, michezo saba tu baada ya kuanza msimu mpya.

Kibarua cha Tuchel kimeota mbawa siku moja baada ya Chelsea kuchapwa bao 1-0 na Dinamo Zagreb katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi.

Chelsea pia imepoteza michezo miwili kati ya sita ya ufunguzi wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu na ipo nyuma kwa pointi tano nyumba ya kinara Arsenal.

Taarifa ya klabu hiyo imesema: “Kwa niaba ya kila mmoja katika Klabu ya Chelsea, klabu ingependa kutoa shukrani zake kwa Thomas Tuchel na benchi lake kwa juhudi zao wakati wakiwa timu hii.

“Wakati wamiliki wapya wanafikisha siku 100 tangu kununua klabu na wakati wakiendelea na jitihada za kuinua klabu, wamiliki wapya wanamini sasa wakati sahihi kufanya mabadiliako haya.”

Kocha wa timu ya kwanza Anthony Barry anatarajiwa kuwa kocha wa muda wa Chelsea hadi mbadala wa Tuchel atakapoteuliwa.

Tuchel was initially appointed in January 2021 and led the club to Champions League success just five months later.

Tuchel aliteuliwa Januari 2021 na aliiongoza klabu hiyo kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya miezi mitano baadaye.

Alishinda michezo 60 kati ya 100 akiwa Kocha Chelsea akifanikisha ubingwa wa Kombe la Klabu Duniani 2021 na kufika fainali ya Kombe la FA mara mbili.

Ripoti zimesema Mauricio Pochettino, Zinedine Zidane na Graham Potter wanapewa kipaumbele kuchukua nafasi ya Tuchel.

Related Articles

Back to top button