Chelsea, Caicedo wakubaliana vipengele binafsi

KLABU ya Chelsea imeripotiwa kukubaliana vipengele banafsi na nyota wa Ecuador, Moises Caicedo lakini itahitajika kutatua suala la ada na Brighton iwapo ina nia ya kumpeleka Stamford Bridge.
Wiki iliyopita Chelsea ilipanga kuimairisha mazungumzo kwa ajili ya kumsajili Caicedo baada ya ofa ya ada ya pauni milioni 60 sawa na shilingi bilioni 183.3 kukataliwa wiki mbili zilizopita.
Brighton inataka zaidi ya pauni milioni 80 sawa na shilingi bilioni 244.5 ili kumwachia nyota wake huyo.
Hatua ya Chelsea kutaka kumsajili kiungo huyo wa Ecuador imekuja baada ya NG’olo Kante kukamilisha uhamisho kwenda Al-Ittihad ya Saudi Arabia wakati Mateo Kovacic anakaribia kwenda Manchester City na Mason Mount anatarajiwa kujiunga na Manchester United majira haya ya joto.