Chai yamponya dada wa muigizaji ugonjwa wa ini

MUMBAI: DADA wa muigizaji wa filamu za Bollywood, Hrithik Roshan, Sunaina Roshan ameweka wazi kwamba chai imemsaidia kuondokana na ugonjwa wa mafuta ya ini uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Mwaka 2007, aligundulika kuwa na saratani adimu iliyoathiri kizazi chake na pia aligundulika kuwa na ugonjwa wa ini lenye mafuta mengi.
Katika mahojiano yake hivi karibuni alisema: “Hata kabla sijagunduliwa na homa ya manjano, wiki moja kabla ya viwango vyangu vya sodiamu kupungua nilitundikiwa dripu,
“Pia nilipogunduliwa kuwa na ini yenye mafuta mengi, sikuwa makini na afya yangu, sikufanya mazoezi na sikuacha kula vyakula nilivyokatazwa kula na daktari, sikujali kabisa,” aliongeza.
Sunaina alifichua kwamba kwa kufuata lishe bora iliyopendekezwa na mtaalamu wa lishe, Ryan Fernando, kuondoa vyakula vilivyodhuru ini lake, na kunywa chai ya detox kama vile chamomile, dandelion na chai ya nettle, ilimsaidia ini lake likatoka daraja la 3 hadi daraja la 1. Baada ya hapo, alifuata utaratibu wa kurejesha utumbo, na akaondoa kabisa ini lenye mafuta.
“Mwaka jana, nilipofanya vipimo kadhaa, SGPT yangu na SGOT vimeng’enya vya ini vilivyojaribiwa katika ripoti za damu ili kutathmini uharibifu wa ini zilitoka juu. Daktari wangu alipendekeza nifanye sonography. Nilizingatia sana mazoezi na kula niliacha kula vyakula vya mafuta.”
Hata hivyo, vipimo viliporudi, daktari wake alitangaza habari njema kwamba mafuta katika ini lake yamepotea, “Siku hiyo, nililia sana sikuamini zaidia ya kufikiria kifo kwa muda mwingi’.”