EPL

Bournemouth yamnasa winga wa Leverkusen

BOURNEMOUTH: KLABU ya Bournemouth imetangaza kumsajili winga Amine Adli kutoka Bayer Leverkusen kwa ada ambayo vyombo vya Habari vya England vinasema inaweza kupanda hadi Pauni milioni 25.1.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ni mchezaji wa saba kusajiliwa na Bournemouth yenye jina la utani la ‘Cherries’ kwenye dirisha hili la usajili na amejiunga kwa mkataba wa miaka mitano.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco kimsingi hucheza kama winga wa kushoto lakini pia amemeonekana kuimudu vyema nafasi ya namba 10 lakini pia upande wa kulia.

Adli aliichezea Leverkusen mechi 143, akifunga mabao 10 na kutoa asisti 12 katika michezo 42 mnamo 2023-24 huku wakishinda mara mbili ya Bundesliga na Kombe la Ujerumani chini ya meneja wa zamani Xabi Alonso.

Bournemouth sasa imetumia takriban pauni milioni 350 kufanya usajili chini ya mmiliki mpya bilionea Mmarekani Bill Foley, ambaye alichukua klabu hiyo kabla ya dirisha la Januari 2023.

‘The Cherries’ pia wamewauza wachezaji kadhaa kama mabeki Milos Kerkez, Dean Huijsen na Illia Zabarnyi wote wakiondoka kwa jumla ya pauni milioni 150 kwenda Liverpool, Real Madrid na PSG kwenye dirisha hili.

Bournemouth wanakaribia kukamilisha biashara yao ya usajili dirisha hili na wanalenga kumnasa kwa mkopo beki wa Chelsea Axel Disasi ambaye ‘The Blues’ wangependa kumuuza mazima.

Related Articles

Back to top button