AFCON

Biteko: Iungeni mkono Taifa Stars

DAR ES SALAAM: SERIKALI imewaomba wadau wa soka kuunga mkono timu ya taifa ‘Taifa Stars’ katika maandalizi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa  wachezaji wa ndani  ‘CHAN’ yatakayofanyika Agosti mwaka huu itakayofanyika nchini Tanzania, Kenya na Uganda.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko alipofungua Kongamano la wadau wa michezo kuelekea CHAN 2024 na AFCON 2027.

Dk. Biteko amesema  wadau wanapaswa kuunga mkono maandalizi ya timu ya taifa ili ijiandaee vyema na michuano hiyo.

“Wito kwa wadau wa soka na Watanzania kiujumla kuiunga mkono timu yetu ya taifa katika maandalizi ya CHAN, pamoja na kutoa rasilimali katika kuwezesha timu hiyo kipindi cha maandalizi,” amesema.

Biteko ameongeza  kuwa ili timu ifanye vyema inatakiwa kusapotiwa na kuipatia hamasa kipindi inacheza.

“Watanzania wanapaswa kujitokeza uwanjani kwa wingi kwenda kuipa hamasa na kuunga mkono  timu ya taifa ili ifanye vyema hadi kufika hatua ya fainali.

“Michuano ya CHAN na AFCON inaleta fursa mbalimbali kwa watanzania, utalii katika hifadhi zetu,  usafirishaji,  malazi (hotel) na sehemu za burudani kutokana na idadi ya wageni watakaokuja,” amesema.

Related Articles

Back to top button