EPLKwingineko

Bil 155/- zampeleka Nkunku Chelsea

KLABU ya Chelsea imemsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Christopher Nkunku kwa pauni 52 sawa na shilingi bilioni 155.5 kutoka RB Leipzig ya Ujerumani.

Nkunku ambaye amecheza michezo 10 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa ni usajili wa kwanza wa Kocha Mauricio Pochettino wa Chelsea tangu aanze kukinoa kikosi hicho mwezi uliopita.

“Nina furaha sana kujiunga na Chelsea. Juhudi kubwa ilifanywa kunileta kwenye klabu hii. Nimefurahishwa sana na changamoto hii na nitajivunia kuvaa jezi ya Chelsea,”amesema Nkunku wakati akizungumza na tovuti ya klabu hiyo.

Nkunku mwenye umri wa miaka 25 amefunga magoli 16 katika michezo 25 msimu uliopita wa Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.

Pia alikuwa wa mchezaji bora wa msimu kwa wachezaji wa kulipwa msimu wa 2021-22 baada ya kufunga magoli 20 na kusaidia 15 katika ligi.

Related Articles

Back to top button