Muziki

Bien: Kuwa Solo ulikuwa mpango wangu wa pili

NAIROBI: MWIMBAJI wa Kenya Bien Baraza, ambaye zamani alikuwa mmoja wa waimbaji wanne wa bendi maarufu ya Sauti Sol, ameweka wazi kwamba kuimba mwenyewe (solo) ulikuwa mpango wake wa pili baada ya kuimba na katika bendi ya wanamuziki wengi.

Bien amekuwa msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kupamba jukwaa la kipindi cha redio cha The Breakfast Club huko New York, tamasha ambalo linaweka jina lake miongoni mwa watu mashuhuri wa muziki barani humo.

Akizungumzia uamuzi wa kupanga njia yake mwenyewe mbali na Sauti Sol baada ya safari ya miongo miwili pamoja, Bien amesema; “Huu ni mpango wangu wa pili wa maisha. Nilikuwa katika bendi ya wanamuziki wanne kwa miaka 20. Sasa mimi ni msanii wa solo. Nimekuwa peke yangu kwa miaka miwili sasa na kila kitu kinakwenda vizuri.”

Katika ziara ya majimbo kumi ya Marekani aliyotembelea na kuimba sio tu anawapa Wamarekani ladha bora zaidi ya Afrika Mashariki, lakini pia anajitambulisha tena si tu kama mwimbaji, lakini kama mtu aliyezaliwa upya katika muziki.

Akizungumzia kilichosababisha akatoka nje ya bendi ya Sauti Sol anasema; “Sote tunafanya kazi pamoja. Sote tunaandikiana na tunafanyakazi pamoja hatuna shida yoyote tupo sawa,” ameeleza.

Akizungumzia azma ya serikali ya Kenya yenye utata ya kuandaa tuzo za Grammy za Afrika amesema habari zilitoka wakati mbaya kwa sababu kiuchumi, na hata sasa Kenya hatufanyi vizuri kama nchi. Kwa hivyo dola milioni 3.8 zilizotumiwa kwenye Grammys zinahisi kama matumizi ya msukumo kwa watu,” alisema.

Related Articles

Back to top button