Mahusiano

Ben Affleck amzungumzia ‘ex wake’ Jennifer Lopez

NEW YORK: LICHA ya kuachana kati ya waigizaji Ben Affleck na Jennifer Lopez Ben bado wawili hawa wanaheshimiana mno kiasi kwamba Ben Affleck amemsifu ex wake Jennifer kwa upekee wake kipindi chote walichokuwa katika mapenzi yao.

Affleck amemwaga sifa hizo za ex wake huyo wakati wa uzinduzi wa onesho la kwanza la Los Angeles la ‘The Accountant 2’.

Katika onesho hilo Affleck aliwaambia waandishi wa habari kuwa katika hafla hiyo aliambatana na watoto wake pamoja na wa ex wake huyo.

“Ni usiku mzuri sana. Watoto wako hapa, watoto wa Jen wako hapa. Nimefurahi sana. Ninajivunia filamu, napenda filamu na napenda watoto wote, inasisimua,” amesema.

Watoto wa Ben na mke wake wa kwanza, Jennifer Garner ni Violet mwenye miaka 19, Seraphina mwenye miaka 16, na Samuel mwenye miaka 13, wakati Jennifer Lopez mwenye miaka 55, na mume wake wa zamani Marc Anthony ni mapacha Max na Emme wenye miaka 17.

“Sisomi vitu mtandaoni sana, na wakati mwingine ninapata hisia kwamba watu wanaendeleza mambo mabaya. Kwa rekodi, Jennifer Lopez anavutia mno, alikuwa mwanamke mzuri kwa watoto wangu na anauhusiano mkubwa anaoendelea nao. Ninawapenda watoto wake yeye ni mtu muhimu sanawametaka kuja name.

Ninafurahi kwamba watoto wako hapa na watoto kama hao, ni furaha ya maisha yangu, na ninafurahi kwamba wametaka kuja name katika uzinduzi wa filamu hii.

Aliongeza kuwa “anajaribu kila awezalo” kuwa baba mzuri kwa watoto wake na aendelee kuwapenda watoto wa ex wake.

Hadithi ya mapenzi ya Jennifer Lopez na Ben Affleck ilianza mapema miaka ya 2000, kabla ya kuachana siku chache kabla ya harusi yao.

Walianzisha tena uchumba wao mnamo 2021 na mwishowe walifunga ndoa mnamo 2022. Baada ya miaka miwili kwenye ndoa yao, Lopez aliwasilisha kesi ya talaka mnamo Agosti 20, kuashiria mwisho wa uhusiano wao.

Kulingana na jalada hilo, wanandoa hao walikuwa wametengana tangu Aprili 26, 2024.

Related Articles

Back to top button