World Cup

Bao bora Kombe la Dunia

BAO la mshambuliaji wa Brazil, Richarlison de Andrade maarufu Richarlison alilofunga dhidi ya Serbia limechaguliwa kuwa bao bora la Kombe la Dunia 2022.

Mshambuliaji huyo wa Tottenham alifunga bao hilo la staili ya ‘mkasi’  dakika ya 73 katika mchezo wa ufunguzi wa timu yake iliposhinda mabao 2-0 kwenye michuano hiyo Novemba 24.

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) limetangaza kuwa mashabiki wamechagua bao hilo wakati wa michuano iliyofanyika Qatar.

Hata hivyo safari ya Brazil Kombe la Dunia iliishia robo fainali baada ya kutolewa na Croatia kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Related Articles

Back to top button