Mahusiano

Bahati athibitisha tarehe ya ndoa

NAIROBI: MWIMBAJI wa Kenya Kevin Bahati na mkewe, Diana Marua, hatimaye wamethibitisha tarehe ya harusi yao ambayo imetarajiwa kwa muda mrefu na wao wenyewe Pamoja na mashabiki zao.

Kutokana na habari hizo mashabiki zao wamewamwagia jumbe za pongezi huku wakiisubiri kwa hamu siku hiyo maalum kwa wanandoa watarajiwa hao.

Jana Bahati aliingia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kufichua tarehe rasmi ya harusi yao akiitaja tarehe 22 bila kuweka mwezi wala mwaka wa harusi hiyo itakapofungwa.

Akiwatania mashabiki, aliandika, “Harusi rasmi ya kihistoria ya Bahati ni tarehe 22… Guess the month?”

Wakati tangazo hilo limezua msisimko, wengine wanasalia na shaka kutokana na kuwahi kutangazwa kama hivyo lakini wanandoa hao watarajiwa walihairisha zoezi hilo na sasa ni awamu nyingine.

Mnamo Juni 2023, Bahati alitangaza kufunga ndoa Desemba 12, 2023, wanandoa hao baadaye walipanga tena Oktoba 2024, kulingana na mwezi wao wa kumbukumbu. Walakini, Bahati alifichua katika mahojiano yake ya Septemba kwamba mpenzi wake Diana hakuwa amepanga tarehe ya tukio hilo.

“Tulikuwa tumepanga harusi yetu
Oktoba 20, lakini Diana aliendelea kuiahirisha. Si juu yangu tena,” Bahati alijitoa akimlaumu Diana kuhairisha mara kwa mara.

Pia amesema kwamba Diana alikuwa akizingatia tarehe ya Februari lakini alisita kutoa tangazo lingine mapema.

“Sasa anazungumza juu ya tarehe ya Februari, lakini nitamngojea kuifanya rasmi. Nimetoa matangazo ya kutosha,” ameeleza Bahati.

Related Articles

Back to top button