Habari Mpya

Azam yaanza kusaka kocha mpya

MTENDAJI Mkuu wa Azam, Abdulikarim Amin ‘Popat’ amesema mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayerithi mikoba ya Abdulihimid Moallin umeanza.

Akizungumza na Spotileo Popat amesema Azam inataka kocha mwenye vigezo zinavyoendana na malengo ya klabu msimu huu ambayo ni ubingwa katika michuano yote wanayoshiriki.

“Tumeanza kupokea maombi CV, kutoka sehemu mbalimbali na baada ya hapo tutaanza kuzichambua ili kupata kocha mwenye vigezo tunavyovihitaji,” amesema Popat.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa mchakato huo wataufanya kwa haraka sababu timu ipo kwenye mashindano ya ligi na hivi karibuni wanatarajiwa kuanza kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa sasa kikosi cha Azam kipo chini ya kocha Kally Ongala ambaye alikuwa kocha wa washambuliaji.

Agosti 29 Azam ilfikia makubaliano ya pande mbili na kocha Abdihamid Moallin na msaidizi wake, Omary Nasser kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia.

Hata hivyo ilisema makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi katika klabu hiyo kwenye nafasi nyingine ambazo zitazitangazwa baadaye.

Related Articles

Back to top button