Nyumbani

Azam FC yaanza na muundo mpya

DAR ES SALAAM: KLABU ya Azam FC imetangaza mabadiliko ya muundo wa uongozi wake ambayo yanaanza msimu huu.

Mabadiliko hayo ni ya muundo wa kiutawala ambapo hivi sasa itakuwa inaongozwa na Rais wa Klabu na sio mwenyekiti tena.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa klabu hiyo, aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Nassor Idrissa kwa sasa atakuwa Rais.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amepanda cheo na sasa anakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

“Rais wa klabu atakuwa na makamu wawili: Makamu wa Rais anayeshughulika na timu kubwa, nafasi hii itashikwa na Popat.

“Makamu wa Rais anayeshughulika na akademi ambapo nafasi hii itashikwa na Omary Kuwe.

“Kutokana na mabadiliko haya, nafasi ya Mtendaji Mkuu (CEO) itajazwa baadaye. Kwa sasa, Abdulkarim Nurdin, ataikaimu hadi atakapopatikana mtendaji mwingine,”ilisema taarifa hiyo.

Mkurugenzi wa Fedha, Abdulkarim Shermohamed, ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi.

Related Articles

Back to top button