La Liga
Atletico Madrid inajinoa tu!
Klabu ya Atletico Madrid imetangaza kumsajili kiungo wa Chelsea, Conor Gallagher baada ya vuta n’kuvute ya wiki kadhaa kati ya klabu hizo mbili.
Kiungo huyo amesajiliwa kwa ada ya pauni milioni 34 baada ya kutokuwa na mahusiano mazuri na uongozi wa chelsea.
Gallagher,24, alihusishwa kutua Aston Villa mapema mwezi huu lakini ni Atletico Madrid ndio iliofanikiwa kumnasa huku ikiwa imeshafanya usajili wa maana wa Julian Alvarez kutoka Manchester City pamoja na mfungaji bora wa pili wa La Liga msimu uliopita, Alexander Sorloth kutoka Villareal.