Kwingineko

Arteta: sina wasiwasi na nafasi za kufunga

LONDON: Meneja wa Washika mitutu wa jiji la London Arsenal Mikel Arteta amesema hana wasiwasi na kikosi chake kutotengeneza nafasi za kufunga mabao kupitia katikati ya uwanja yaani ‘open play’.

Kauli hiyo ya Arteta inakuja baada ya kuwepo kwa ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka ambao wameonesha wasiwasi wao juu ya klabu hiyo siku za hivi karibuni kupata ushindi mara nyingi kupitia mipira ya adhabu.

Arsenal wamekuwa mabingwa wa mipira ya adhabu wakiwa na idadi ya juu zaidi ya mabao 23 yaliyotokana na mipira ya kona tangu kuanza kwa msimu uliopita.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Monaco, Arteta amedai kuwa utaalam huo wa kikosi chake unatokana na kiwango kizuri cha mchezo wa ndani ya uwanja hali inaopelekea wao kulazimisha wapinzani kufanya makosa na kuyatumia kuwaadhibu.

“Sina wasiwasi kwa sababu niliutazama tena mchezo dhidi ya Fulham hatukufanya tofauti sana na walichofanya kwenye ‘open play’. Sijui mnataka tufanye nini, na kwa sababu mipira ya adhabu ni matokeo ya makosa tunayofanya wakati wa kulinda au kushambulia”

“Tunataka kutengeneza nafasi kutokana na kila kitu, mipira ya adhabu pia, tungetengeneza nafasi nyingi na tungeweza kutumia pengine tungefunga goli au hata mawili” amesema Arteta

Arsenal wamekuwa hatari zaidi kwenye mipira ya adhabu na wameanza kuzingatiwa baada ya kuibamiza Manchester United 2-0 magoli yote yakitokana na kona

Related Articles

Back to top button