Kwingineko

Arsenal vs PSG ni swali, kazi, jibu

LONDON:HATIMAYE ule mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka Afrika Mashariki ambao kitakwimu wengi ni mashabiki wa Washika mitutu wa jiji la London, Arsenal, utapigwa leo katika dimba la Emirates pale jijini London nchini England majira ya saa 4 usiku.

Arsenal wanacheza hatua ya nusu fainali baada ya kuwaondosha Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Real Madrid katika mchezo ambao wengi hawakuamini kutokana na kutotabirika kwa Real Madrid hasa katika michuano ya UEFA Champions League.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amesema dhamira yake ni kukivusha kikosi hicho katika hatua hii na kukipeleka kwenye hatua ya fainali na hatimaye kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Kwa upande wake kocha wa PSG Luis Enrique ameahidi kutoa upinzani mkubwa kwa Arsenal akisema yaliopita mwezi Oktoba ni ya zamani na sasa kikosi chake ni kipya na kimepata hamasa baada ya kushinda taji la ligi ya nyumbani Ligue 1.

Hii ni mara ya pili kwa miamba hii kukutana kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kukutana mwezi Oktoba mwaka jana na PSG kupotea mabao 2-0 magoli ya Kai Havertz na Bukayo Saka. Je PSG wamelielewa swali la Arsenal wamelifanyia kazi na sasa wako tayari kutoa majibu au Arsenal wataongeza maswali kwa PSG?

Related Articles

Back to top button