Arijit Singh kuacha kuimba nyimbo za filamu

MUMBAI: Mwanamuziki wa India Madhubanti Bagchi ametoa maoni yake kuhusu uamuzi wa mwanamuziki maarufu Arijit Singh aliyetangaza kuachana na uimbaji wa nyimbo za filamu.
Akizungumza katika mahojiano, Bagchi alisema tasnia ya uimbaji wa filamu mara nyingi huwaweka waimbaji katika makundi maalumu na kuwazuia kufanya ubunifu wao binafsi.
Alieleza kuwa mara nyingi waimbaji hulazimika kuimba aina fulani ya nyimbo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watayarishaji wa filamu, na pale wanapotaka kufanya kazi zao binafsi, mara nyingi nyimbo zao hazipewi kipaumbele wala kuwekewa uwekezaji mkubwa wa kifedha.
Kauli hiyo inakuja miezi michache baada ya Arijit Singh kutangaza kustaafu uimbaji wa nyimbo za filamu, uamuzi uliowashangaza mashabiki wengi wa muziki nchini India.




