La Liga

Arbeloa: Haijulikani lini Mbappe atarudi kucheza

MADRID: KOCHA wa Real Madrid, Álvaro Arbeloa, amesema hali ya Kylian Mbappé imeanza kuimarika baada ya kuumia goti la kushoto  licha ya kutokuwa muda sahihi wa nyota huyo kurejea.

Mbappé amekuwa nje ya uwanja kutokana na kukabiliwa na majeraha hayo yanayomsumbua tangu Desemba.

“Ninasalimiana naye kila siku,” Arbeloa alisema katika mkutano na waandishi wa habari. “Hali yake iko chini ya udhibiti, kila siku anakuwa bora. Ni mchakato ambapo tunapita siku baada ya siku kulingana na hali yake. Hivi sasa, ni habari njema zote.”

Mbappé atalazimika kukosa baadhi ya michezo ijayo ambapo mbele yao kuna mechi ya LaLiga dhidi ya Celta Vigo Ijumaa, mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City, mechi ya ligi na Elche, na kisha mechi ya marudiano dhidi ya City Machi 17.

Madrid pia wanamkosa nyota wao, Jude Bellingham, anayetarajiwa kurudi Aprili baada ya kupona jeraha la misuli ya nyonga. Mbappé na Bellingham walisafiri hivi karibuni kwenda Ufaransa na Uingereza kwa ushauri wa kitabibu, huku Madrid ikithibitisha madaktari wa Ufaransa wanaunga mkono matibabu ya tahadhari waliyochagua kwa Mbappé.

Madrid imepoteza mechi mbili mfululizo za LaLiga, zikishindwa na Osasuna na Getafe, lakini Arbeloa amesema hawataacha kupambana.

“Kwa timu kama Madrid, kupoteza mechi daima ni jambo gumu, Ni pointi nne, tutaendelea kupigana,”amesema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button