La Liga

Arbeloa alamba dili Madrid

MADRID: MABINGWA wa kihistoria wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya wamemteua beki wao zamani Alvaro Arbeloa kuchukua nafasi ya kukinoa kikosi cha timu tanzu ya Real Madrid Castilla inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Hispania akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Raul Gonzalez.

Arbeloa anachukua nafasi hiyo wakati huu ambao Castilla imemaliza ligi hiyo maarufu kama Primera Federacion katika nafasi ya sita ikikosa hata nafasi ya kucheza ‘playoffs’ za kuipandisha ligi daraja la pili nchini humo kwa msimu ujao.

Uongozi wa Madrid unaamini beki wao huyo wa zamani anao uwezo wa kuisaidia klabu hiyo kupata makali inayoyahitaji kupanda madaraja na hatimaye kuifikia LaLiga katika siku za usoni huku taarifa zikieleza Arbeloa hatakuwa na presha kwa sababu viongozi hao wanatafakari namna ya kuwa na timu mbili kwenye ligi kuu

Pamoja na mengine Arbeloa anahistoria ya kuwa mshindi wa Kombe la Dunia la 2010 pamoja na makombe mawili ya Euro huku akishinda taji moja la LaLiga na mawili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kabla ya kustaafu mwaka 2017 na kurejea viunga vya Bernabeu 2020 kuifundisha timu ya U17 na timu ya U19 mwaka 2022.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button