Familia

Aquaman awakataza watoto wake kutumia simu & TV

Awataka wawe wabunifu

LOS ANGELES: Nyota wa Hollywood, Jason Momoa, maarufu kwa kucheza Aquaman, amewakataza watoto wake kutumia simu, TV, na kujihusisha na michezo ya video. Badala yake, amewataka wawe wabunifu wao wenyewe.

Kabla ya onesho la kwanza la filamu ya Minecraft Aquaman, Momoa ameweka wazi kuwa watoto wake wataingia katika ulimwengu wa kidijitali wanapokuwa watu wazima tu.

“Hatuna TV,” amesema.
“Mwanangu hana hata simu. Ana umri wa miaka 16 na hana simu. Sisi ni tofauti. Anapofikisha miaka 18 na kuondoka nyumbani, anaweza kuchunguza ulimwengu huo,” ameongeza Aquaman.

“Ninataka tu watumie ubunifu wao kwa njia tofauti,” aliongeza, akisisitiza kwamba familia yake inajishughulika na shughuli za mikono badala ya kutazama skrini bila akili.

“Watu walikuwa wazuri tu kabla ya simu. Hakuna aliyeambiwa la kufanya, na ilibidi ujue bila kuwa na simu,” amesisitiza.

Hata hivyo, Momoa hapingani kabisa na muda wa TV. Yeye na watoto wake hutazama sinema pamoja kama familia na si vinginevyo.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii waliunga mkono msimamo wake. “Wazazi wengi husukuma iPad na simu kwa watoto wao kama njia ya uvivu kwa mzazi,” mtoa maoni mmoja aliandika.

Mwaka jana, shule moja katika jiji la Los Angeles ilipiga marufuku matumizi ya simu wakati wa saa za shule, ikitaja wasiwasi kuhusu wanafunzi wanaotumia simu kutokuwa na uwezo wa kuzingatia na kuingiliana katika maisha halisi.

Related Articles

Back to top button