Mastaa

Anjella: Mungu Ndiye Kila Kitu Kwenye Maisha Ya Mwanadamu

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Angella Samson, ameeleza kuwa Mungu ndiye kila kitu katika maisha ya mwanadamu, akionyesha wazi imani yake kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Anjella ameposti picha mpya iliyoambatana na maneno ya kutafakari kuhusu nguvu na mamlaka ya Mungu.

Katika ujumbe wake ameandika:“Kule Misri uliwatoa na Kanaani ukawapeleka. Falme zote zilizosimama ulipokuja wewe ziliinama. Huyu ndiye MUNGU mwenye mamlaka.” Anjella

Ujumbe huo umeibua mijadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakijiuliza kama msanii huyo alikuwa akitoa dongo kwa mtu fulani au akionyesha tu ishara ya shukrani na imani ya kiroho.

Hata hivyo, hadi sasa Anjella hajatoa ufafanuzi zaidi kuhusu kilichomsukuma kuandika maneno hayo, huku mashabiki wake wakisubiri kuona kama ni mwanzo wa ukurasa mpya katika maisha yake binafsi au kisanaa.

Related Articles

Back to top button