Angelina Jolie katika penzi jipya

LOS ANGELES: MCHEZA sinema Angelina Jolie anadaiwa kuingia tena katika uhusiano wa kimapenzi na Johnny Depp baada ya kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja wakijadiliana katika mikutano ya faragha.
Johnny Depp na Angelina Jolie wamekutana na kuzungumza kwa muda mrefu huko London Uingereza na Los Angeles, Marekani Jarida la Star limeripoti.
Mwanzo huo mpya unadaiwa unakuja baada ya mvutano wa kisheria wa Jolie na mume wake wa zamani Brad Pitt kuongezeka huku jolie akionekana mwenye furaha sana.
Licha ya hayo yote lakini taarifa zaidiazinaeleza kuwa Depp yuko wazi katika hilo lakini Jolie anaonekana kusitasita huku akiwa na ulinzi mkali kila anapokuwa ili kukwepa maswali ya waandishi wa habari.
Watu wa karibu wa Johnny wanasema Angelina Jolie anafanana mno na aliyekuwa mke wa Johnny, Amber Heard. Ndiyo maana Johnny amekuwa wazi mno kuliko Angelina.