Africa

TP Mazembe kumsajili golikipa msenegali

GOLIKIPA wa timu ya taifa ya Senegal Alioune Badara Faty anatarajiwa kujiunga na miamba ya soka ya Jamhuri ya Kimokrasi ya Congo, TP Mazembe.

Alioune anakipiga katika klabu ya Casa Sports yenye makao yake makuu katika mji wa Ziguinchor.

“Nahitaji kupata changamoto mpya. Naamini muda niliocheza Senegal unatosha,”amesema Alioune.

Kwa mujibu wa mtandao wa michezo Wiwsport wa Senegal makubaliano yamefikiwa kati ya Casa Sports na TP Mazembe.

Alioune mwenye umri wa miaka 24 anajiunga na TP Mazembe inayonolewa na kocha kutoka Senegal, Lamine Ndiaye.

Akiwa Casa Sports Alioune Badara Faty ameshinda mataji yote ya mashindano ya ndani na katika timu ya taifa ameshinda Komba la Mataifa ya Afrika(AFCON) na lile la Wachezaji wa Ligi za Afrika(CHAN).

Related Articles

Back to top button