Kwingineko
Alba awafuata Messi, Busquests

BEKI wa Hispania Jordi Albe ataungana na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Lionel Messi na Sergio Busquests katika klabu ya Inter Miami ya Marekani
Rais wa Inter Miami, Jorge Mas amesema beki huyo mwenye umri wa miaka 34 amesaini mkataba na anapaswa kuwepo kwenye kikosi kuikabili Atlanta Julai 26 katika mchezo wa Ligi Kuu, Marekani(MLS).
Alba ambaye ameondoka Barcelona wakati mkataba wake ulipokwisha mwezi uliopita ameitumikia miamba hiyo ya Hispania kwa miaka kumi akifunga magoli 27 katika michezo 459 aliyocheza.
Alisaidia klabu hiyo kushinda mataji sita ya La Liga na la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2025.