Al Nasrr ya Clara Luvanga yatwaa ubingwa

TIMU ya Al Nasrr wanawake anayocheza mchezaji wa Twiga Stars Clara Luvanga imetwaa taji la Ligi Kuu ya Saudi Arabia ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.
Al Nasrr walitangazwa mabingwa jana baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Al Ahly jana huku Clara akitupia bao katika ushindi wa mchezo wa raundi ya 16 na mengine yakifungwa na Nesrine Bahlouli na Ruth Kipoyi.
Mabingwa hao wamefikisha pointi 48 katika michezo 16 huku mpinzani wake Ahly akiwa nafasi ya pili kwa pointi 37 kukiwa na tofauti ya pointi 11.
Mabingwa hao wamebakiza mechi mbili mkononi kukamilisha ratiba ya ligi. Imechukua ubingwa ikiwa haijapoteza mchezo wowote wala kupata sare.
Takwimu za ligi hiyo yenye timu 10 zinaonesha ndio timu pekee haijapoteza mchezo wowote.
Mshambuliaji nyota wa Al Nasrr wanaume Cristiano Ronaldo ameipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa.