Al-Ittihad yawania saini ya Son

KLABU ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia imeripotiwa kuandaa pauni milioni 51 sawa na shilingi bilioni 152.5 kumsajili Son Heung-min, huku nyota huyo wa Tottenham HotsSpur akiwa mchezaji wa hivi karibuni kuhusishwa kuhamia Ligi Kuu ya Pro.
Al-Ittihad tayari imemsajili Karim Benzema kutoka Real Madrid na inatarajiwa kukamilisha dili la N’Golo Kante wa Chelsea.
Mtandao wa Michezo na Burudani(ESPN) wa Marekani umesema Al-Ittihad walimfuata fowadi huyo wa Korea Kusini na kumpa ofa ya mkataba wa miaka minne wenye mshahara wa pauni milioni 26 sawa na shilingi bilioni 77.7 kwa msimu.
Klabu hiyo inatarajiwa kutuma maombi ya awali kwa Tottenham ya pauni milioni 51 pamoja na bonasi kumsajili Son.
Son amefunga magoli 145 katika michezo 372 akiwa Tottenham tangu ajiunga na klabu hiyo akitokea Bayer Leverkusen mwaka 2015.